Skip to content

Feza Boys Students

A visit from charming young boys from Feza boys school. A study tour on learning on industrial activities , professional  needed and investment  technics .

Wanafunzi wa shule ya Sekondari FEZA Boys walipata nfasi ya kutembelea kiwanda cha Hill Group na kujionea kazi zinazofanyika katika utengenezaji wa bidhaa. Waliweza kuona ni jinsi gani kampuni ilivyojikita katika kutengeneza bidhaa bora kwa kutumia mashine za kisasa. Wanafunzai wengi walishangazwa na mashine zinazotumika kutengeneza bidhaa hasa mashine za kutengeneza maji na kujionea mlolongo mzima wa jinsi malighafi zinavyopokelewa, kuhifadhiwa na kutumika katika mashine mbalimbali.

Wanafunzi hawa waliweza kupata chakula cha pamoja kilichoandaliwa na kampuni baada ya ziara yao fupi.

Ukiachana na ziara yao fupi, wanafunzi wa FEZA boys walipata nafasi ya kuongea naMkurugenzi wa Hill Group Mr. Hillary Shoo na kupewa maneno ya ushawishi kwa masomo yanayoyasoma na vitu gani vilimfanyampaka ameweza kufikia hapo alipo.

Pia wanafunzi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na wengi wao walikuwa nashauku ya kujua kwa undani zaidi juu ya biashara zinavyofanyika.